Swahili
Swahili
Brochure 1
Brochure 2
<<

Kwa Bi, Bwana,

Kusema jambo moja-kumaanisha kitu tofauti: kwa watu ambao wanaugua kutokana afasia ni jambo linalofanyika. Afasia inapatikana ulimwenguni kote na inaweza kumpata mtu yeyote. Duniani, zaidi ya watu milioni 5 wanaugua kutokana na ugonjwa huu.

Humu ndani utapata maelezo kuhusu afasia: tata ya lugha inayotokana na dhara ya ubongo, ambayo huwafanya watu wasiweze kuongea, kuelewa, kusoma, ama kuandika kwa njia ya kwaida.

Maelezo haya umepewa bila malipo na Shirikisho la Kimataifa la Afasia. Shirikisho hili linalo wajibu, kati ya mambo mengine, kuwaelimisha watu ulimwenguni kuhusu tata hii ya lugha.

Tumetoa asante kwa bidii za shirika za umma za afasia ambazo zinahusika na mipango hizi za ulimwengu, asante pia kwa msaada mbali mbali za Rotary Clubs, tunaweza kuwapa maelezo haya.
Maelezo haya yanakusudiwa kuwafahamisha wagonjwa na familia zao. Tungependa kuwaomba mweze kueneza maelezo haya katika shirika zenyu ama mhakikishe kuwa yamefika mahali ipasavyo. Hii inaweza kuwa, kwa mfano, idara za neurologia katika mahospitali, idara za urudishaji, kliniki za usemi, ama kikundi cha watu ambao wanavutiwa na wauguzi katika nchi yako.

Tunatumahi kuwa maelezo haya yatakunufaisha; na tunatumahi zaidi kuwa tunaweza kusaidia kuhakikisha kuwa watu wanaougua kutokana na afasia hawadhuriwi na maisha ya upweke. Tutaangalia majibu na shauri zenyu; mnaweza kushauriana na aliye hapo chini kwa maelezo zaidi (afadhali kwa kiingereza).

Salamu, kwa dhati

Shirikisho la Kimataifa la Afasia

Mrs Monique Lindhout.

made possible by Rotary